Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali ameagiza mara moja kuvunjwa mara Moja kikundi cha ulinzi cha Nkiri kinachoeneza chuki kwa wananchi badala ya kudumisha umoja na amani katika kijiji cha Yulansoni tarafa ya Kinyangiri wilayani Mkalama
Ametoa agizo hilo Januari 31,2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Yulansoni tarafa ya Kinyangiri kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanananchi wa kijiji hicho.
"Kuanzia leo sitaki kusikia kikundi cha ulinzi cha Nkiri, marufuku kubaguana, wananchi mkisikia mtu anabaguliwa nipeni taarifa tuwashughulikie, na tutawashughulikia vilivyo" Mhe Moses Machali. Sambamba na hayo Mhe. Moses Machali amewataka wananchi kutii sheria za nchi, na kuahidi kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi hao.
Ziara ya mkuu wa wilaya siku ya tarehe 31/01/2024 ilianzia katika mgodi wa Pubo uliopo katika kata ya Tumuli kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanyika katika mgodi huo ambapo akiwa hapo ameutaka uongozi wa mgodi huo kulipa tozo wanazodaiwa na Halmashauri ya wilaya ya Mkalama pamoja na kuzingatia sheria na kanuni za uchimbaji madini.
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.