Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Bi.Asia Messos amekabidhi jumla ya vitabu 20471 vya darasa la awali, la kwanza na la tatu pamoja na mihutasari ya darasa la tatu hadi la saba kwa shule za msingi wilayani Mkalama vilivyitolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) katika kupunguza upungufu uliopo na kuwezesha watoto kusoma kwa urahisi
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika leo Aprili 3,2024 katika ukumbi wa Sheketela, Mkurugenzi Mtendaji Bi.Asia Messos amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuboresha elimu nchini Tanzania sambamba na kuzitaka shule zilizopokea vitabu hivyo kuhakikisha vinatumika kufundishia kulingana na maelekezo waliopewa
“Tumepokea vitabu 20471 kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) vyenye thamani ya shilingi milioni 24, hizi zote ni jihudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya elimu sambamba na mazingira ya kujifunzia na ufundishaji” Mkurugenzi Mtendaji Bi.Asia Messos
“Nitoe wito kwa walimu kuhakikisha vitabu hivi wanatumia kwa ajili ya kufundishia watoto wetu, Tutakapopita katika shule tusikute vitabu hivi kwenye makabati, vitabu vizuri tukivitumia vizuri tutawezakuinua taaluma wilayani kwetu” Mkurugenzi Mtendaji Bi.Asia Messos
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi, Bi.Jusline G.Bandiko amesema vitababu hivyo vitasaidia kupunguza upungufu uliopo sambamba na hilo, ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu wilayani Mkalama.
Vitabu vilivyotolewa kwa darasa la awali ni vitabu 6,836, darasa la kwanza vitabu 7,932 na darasa la tatu vitabu 5703 na mihutahasari 1378 vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini na nne ambavyo vitabu hivi pamoja na mihutasari vitagawia katika shule 93 za msingi wilayani Mkalama
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.