Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo amepiga marufuku shughuli zote za waganga wa jadi wanaotumia ramli chonganishi (lamba lamba) zinazoendelea wilayani Mkalama kwani zinaashiria uvunjifu wa amani wilayani hapa .
Amesema hayo wakati akitoa salamu za serikalini katika Mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani wa robo ya pili kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 lililofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
Amewataka viongozi wote ndani ya wilaya kuungana na kupinga suala hilo linaloleta uvunjifu wa amani kwani wananchi wamekua wakitozwa fedha ili kuwaleta waganga hao ambao wamekua wakisema wanatoa uchawi kitu kinacholeta taharuki na chuki katika jamii.
"Kazi yetu ni kuhakikisha usalama wa raia na Mali zao ,kuanzia Leo ninatoa tamko kwenye baraza hili la madiwani sitaki kusikia suala la lamba lamba linaendelea ndani ya wilaya kwa yeyote atakayehusika na kuwaleta hao lamba lamba hakutakua na msamaha kwakweli, kama wewe unataka kumuabudu huyo lamba lamba ufanye kimya kimya huko nyumbani kwako sio kuwalazimisha watu wengine tena wa Imani tofauti tofauti" .Aliongeza Dc Kizigo.
Pia amesema kuwa Nchi hii inaongozwa Kwa kufuata katiba na Sheria hivyo hatavumilia viashiria vya uvunjifu wa amani unaosababishwa na lamba lamba ambao wanakiuka maagizo ya serikali kwa kulazimisha kuingia kwenye nyumba za watu wakidai kuwa wanatoa uchawi kinyume na utaratibu wa Sheria za Nchi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.