• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

DC MACHALI AWATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA KAZI

Imewekwa kwenye: February 9th, 2023



Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali amewataka Watumishi wa Idara zote na Vitengo na Taasisi zilizopo Mkalama kila mmoja kwa nafasi yake  kufanya kazi kwa weledi, kuacha mzaha, kuheshimu kazi huku wakizingatia  Sheria na Taratibu zilizowekwa katika kufuata  maelekezo halali wanayopewa yasiyo athiri taratibu za kazi.


Ameyasema hayo mapema leo February 9, 2023 katika  kikao kazi kilichojumuisha, Wakuu wa Idara, Vitengo, Taasisi na Watendaji wa Kata katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mkalama kikiwa na lengo la kukumbusha majukumu na wajibu wa kila mmoja  kufanya kazi kwa bidii  kwa kuzingatia Taratibu na Sheria za kazi.

‘’Tumekuja hapa kukumbushana ni nini tunachotakiwa kufanya, kupeana muelekeo bila kutoka nje ya Misingi iliyojengwa kwenye Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ Alisisitiza Mhe. Machali.


Mhe. Machali, ameongeza kuwa kila mmoja kwa nafasi yake ya taaluma anatakiwa kufanya majukumu kwa  weledi na kwa kushirikiana pia kuwa tayari kupokea mabadiliko ya kifkra ya  namna dunia inavyoenda kutokana na kukua kwa Sayansi na Tekinolojia .


Pamoja  na hayo, aliwataka kutumia nafasi zao kutatua changamoto za Wananchi  kwa kwenda Vijijini kubaini Migogoro ya Ardhi  na namna walivyoishughulikia pia kutoa elimu kwa jamii  kushiriki katika shughuli za Maendeleo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali.


‘’wakuu wa Idara tokeni ofisini  nendeni kwa Wananchi mkashughulikie  matatizo ya Wananchi, ipende na kuiheshimu nafasi yako uliyonayo na kuitendea haki ‘’ Aliongeza Mhe. Machali.


Sanjari na hayo  Mhe. Machali alimwelekeza Mkurugenzi Mtendaji kushirikiana na Timu yake kuhakikisha wanaongeza ukusanyaji wa mapato na kudhibiti mianya yote ya utoroshaji na ukwepaji wa kulipa kodi  Pamoja na kuwataka wakandarasi wanaopata tenda Wilayani hapa kuhakikisha wanalipa ushuru wa Madini ya Ujenzi.


"Mkurugenzi hakikisha unaweka utaratibu mzuri na timu yako kufuatilia ushuru wa kila chanzo, nimeambiwa hapa mna vyanzo kumi na saba(17) vya mapato kama ni mnadani hakikisheni mnakusanya kikamilifu, kama ni Magetini  hakikisheni mnasimamia vizuri’’ Alisema Mhe. Machali


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia Messos ameahidi kushughulikia maelekezo yote waliyopewa leo na Mkuu wa Wilaya  ili kuendana na dira na kasi yake  na kuhakikisha anawaelekeza Menejimenti yake kushughulikia kero za Wananchi kwa ustawi mpana wa wanamkalama.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.