Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewataka wakuu wa Idara na Vitengo kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuacha kukwamisha juhudi za Serikali katika kutelekeza miradi ya maendeleo wilayani hapa.
Ametoa wito huo mapema leo 13/12/2010 katika kikao kazi na wakuu wa Idara na Vitengo,Watendaji wa Vijiji na Kata,pamoja na walimu wakuu wenye miradi,,uliofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Aidha amesisitiza uwajibikaji kila mmoja kwa nafasi yake ili kuhakikisha fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali ya awamu ya Sita zinasimamiwa vizuri na kukamilika kwa wakati
“Pesa tumepokea toka mwezi wa saba, mpaka leo mifumo inasumbua.Mnasingizia mfumo mfumo, kumbe tatizo ni wewe. Acheni kupoteza muda kufanya kazi vitu ambavyo havina tija. Hata kama muda wa kazi umeisha jifunzeni. Msitukwamishe”, Mhe Moses Machali
Mhe, Machali amewaagiza watendaji pamoja na walimu wenye miradi kuhakikisha ifikapo Januari 5, 2024 majengo yote ya shule, vyoo yawe yamekamilika na kuwaagiza kuongeza idadi ya mafundi ili kuharakisha kazi hizo ambapo amewataka kukabidhi miradi hiyo tarehe 5,1-2023 .
Mbali na hilo, Mkuu wa wilaya amewataka pia waratibu wa elimu kubadili tabia zao katika kutekeleza majukumu yao ya kusimamia sekta ya elimu wilayani Mkalama.
“Wachache ambao mnafanyakazi zenu vizuri , wenzangu mabosi, ndio maana tunafeli. Laiti mngelikuwa mnafanyakazi zenu na ndio wanataaluma tusingeendelee kila wakati kuwa mikia, hamfatilii wala kusimamia nidhamu ya walimu, pamoja na miradi” DC Moses Machali
Sambamba na hayo Mhe, Machali amemuagiza Meneja wakala wa Misitu(TFS) kutoa kibali cha ukataji miti kwa vijiji na kata zenye changamoto ya madawati, viti na meza ili waweze kutengeneza mbao na kutatua changamoto hizo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.