Mlkuu wa Wilaya ya Mkalama Mh.Moses Machali amewataka watumishi wa afya wilayani hapa kufanya kazi kwa bidii kwa kuwahudumia vizuri wateja wanaofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Wito huo ameutoa Februari 19/2024 wakati kikao cha Tathimini ya lishe kwa robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/25 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama.
"Nawasihi nendeni mkafanye kazi kwa bidii, kila mmoja atimize wajibu wake. tukifanya kazi kwa bidii tutakuwa tumefikia adhima ya Mhe. Rais Dkt Samia katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma nzuri za afya" DC Machali. Mhe. Machali amewasisitizia pia watumishi hao kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujiunga na bima za afya "nendeni mkafanye hamasa kwa wananchi wajiunge na bima za afya katika maeneo yenu ya kazi" DC Machali
Aidha Mhe. Machali amewataka watendaji kata wilayano hapa kwa kushirikiana na watumishi wa afya kuweka ratiba ya mikutano kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala la lishe, bima za afya pamoja na uzazi wa mpango.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Wilaya ya Mkalama. Bi. Happyness John Sulle amewapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri wanaofanya katika kuwahudumia wananchi wa Mkalama na kuwasisitizia kuendelea kufanya kazi kwa bidii. "Hongereni kwa kazi nzuri mnayofanya, nawasihi tuendelee kuwa na nidhamu katika kazini na kuwajali wateja wetu" DAS Happyness Sulle
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.