Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali amesisitiza suala la Lishe Shuleni ili Wanafunzi waweze kupata chakula kitakachowasaidia kupata muda mwingi wa kujisomea pia kudhibiti Utoro, kujenga afya ya akili kwa mtoto itakayopelekea matokeo chanya na kuleta mapinduzi katika Sekta ya Elimu Wilayani hapa.
Ameyasema hayo mapema leo wakati akiongea na Wananchi wa Kata za Miganga na Nkalakala katika muendelezo wa ziara zake za kusikiliza kero za Wananchi Wilayani Mkalama.
Mhe. Machali amewataka viongozi wa Serikali za Vijijini na Kata kushirikiana na Wazazi kuhakikisha wanaweka mikakati mizuri kwa ajili ya kutoa michango kuwezesha suala la Lishe Shuleni kuhakikisha Afua hiyo inatekelezwa ili Wilaya iwe na Watoto wenye akili timamu kwa Maslahi ya Taifa la kesho.
" Nimewaelekeza Viongozi kuhakikisha wanaweka mikakati ya kutoa chakula Shuleni ili Watoto wapate chakula Shule katika kuongeza ufaulu, kila Mtu anajua ukiwa na njaa huwezi fanya chochote unakuwa na hasira" alisisitiza Mhe. Machali.
Aidha, amezitaka Shule kuhakikisha wanamiliki Ardhi ya kutosha kuanzisha Kilimo cha umwagiliaji Ili kuwezesha upatikanaji wa chakula pamoja na kusaidia kujiendesha yenyewe ikiwa ni pamoja na kutekeleza Afua za Lishe Wilayani hapa.
Sambamba na hayo Mhe. Machali ametoa miezi mitatu kwa Shule zote kuwa na matundu ya vyoo yanayoweza kutosheleza idadi ya Wanafunzi huku akiwataka Wananchi kujitolea nguvu kazi katika kufanikisha shughuli hiyo ambayo pia itapelekea Uhifadhi wa Mazingira.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.