Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali ametoa rai kwa wakulima wilayani Mkalama kujisajili katika mfumo ili waweze kupata mbegu na mbolea za ruzuku
Kauli hiyo ameitoa Desemba 16, 2024 katika kijiji cha Ilunda kata ya Ilunda wakati wa hafla ya kumkabidhi Mshindi wa tuzo ya Mkulima Bora Kitaifa wa Maonesho ya Nane nane 2024 yaliyofanyika katika viwanja vya Nzunguni Jijini Dodoma
“Serikali ilianza na mbolea na sasa imeanza kutoa ruzuku kwenye mbegu za Mahindi na Alizeti,wito wangu kwenu nendeni mkajisali ili muweze kupata mbegu kwa bei nafuu” Mhe. Machali
Akizungumzia suala la utunzaji wa Mazingira, Mhe. Moses Machali amewataka wakazi wa kijiji cha Ilunda kupanda miti katika kupambana na uhalibifu wa mazingira “Lakini naombeni tujitahidi kupanda miti, tukiwa na miti mingi tutapata mvua za kutosha na tutakuwa tumetunza mazingira” Mhe. Machali
Aidha Mhe. Moses Machali amewakumbusha wakazi wa Ilunda na Mkalama ujumla kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa Amani, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujilinda dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.