Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amekemea vikali vitendo vya ushoga, Usagaji na Ubasha Wilayani Mkalama na kuwataka wananchi kujikita kwenye misingi , Imani na Utamaduni wa Mwaafrika .
Ameyasema hayo April 18, 2023 katika ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi katika Kata za Tumuli na Msingi Wilayani Mkalama.
‘’ Haki za binadamu hazipatikani kwakufanya vitendo ambavyo ni kinyume na mapenzi ya Mungu niwaombe viongozi wangu wa dini mliopo hapa hakikisheni kwenye nyumba zenu za ibada mnapinga kwa nguvu zote vitendo hivi ambavyo vinabadili utamaduni wetu ‘’ Aliongeza Mhe. Machali
Pamoja na hayo aliwataka wazazi kukaa na kuongea na Watoto kuhusu madhara ya Ushoga, Ubasha na usagaji kwaajili ya kuwa na kizazi chenye maadili mazuri huku akiwataka kuhakikisha wanasimamia malezi na maadili ya Watoto.
Mhe. Machali aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanashiriki katika shughuli za maendeleo zinatolewa na Serikali ya awamu ya Sita, huku akiwataka kutoa ushirikiano katika kuwabaini wahalifu wote ambao wanatishia amani ya wananchi ambapo amewaahidi jukumu la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanakuwa salama Pamoja na mali zao.
Katika hatua nyingine aliwataka wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali Wilayani Mkalama kuhakikisha wanashughulikia kero na kutatua migogoro yote hususani ile ya Ardhi na mipaka ili kuhakikisha wananchi wanajikita kwenye masuala ya maendeleo na kuachana na migogoro.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.