Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo amesaini Mkataba wa Lishe na watendaji wa Kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama utakaoenda kutekelezwa ngazi ya kata ili kuhakikisha Wilaya inakuwa vizuri kwenye Lishe na kumaliza utapia mlo .
Amesaini Mkataba huo mapema leo Oktoba 27 2022 wakati wa kikao cha tathimini ya lishe , jiongeze tuwavushe salama na iCHF na Watendaji wa Kata katika ukumbi wa uthibiti ubora elimu uliopo katika Halmshauri ya Wilaya ya Mkalama.
Aidha Dc Kizigo aliwataka watendaji , wataalamu wa afya pamoja na wadau wa lishe kuhakikisha wanasimamia zoezi la lishe ili kuandaa kizazi bora cha baadae.
Katika hatua nyingine aliwataka kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa lishe pamoja na faida za kujifungulia hospitali ili kuepusha vifo vya Mama na mtoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji wa Kata kushirikiana na watendaji wa Vijiji kusimamia majumu yao kwa weledi kwakufuata sheria za utumishi wa Umma kuwa waadilifu kwa kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yao.
Hata hivyo aliwataka kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali pamoja na kufuatilia ukamilisha wa shule madarasa mawili (SM2) ili kupunguza uhaba wa madarasa wilayani Mkalama.
Afisa Lishe Wilaya ya Mkalama Eliwandisha Kinyau alisema kuwa wataendelea kutoa elimu shuleni kuhusu masuala ya lishe na ulaji bora unaoshauriwa kwa kufuata makundi matano ya chakula pamoja mna kuanzisha bustani Penseli ya kilimo cha mboga mboga ili kuboresha lishe kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.