Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Peter Masindi amewataka wajumbe wa kamati ya Afya Msingi ngazi ya Wilaya (PHC), Wakuu wa idara na vitengo pamoja na Viongozi wa dini Wilaya ya Mkalama kuhakikisha wanawahamasisha wazazi wenye watoto wa umri wa miezi 9 hadi 59 kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya Ili waweze kupata chanjo ya Surua na Rubella .
Ameyasema hayo mapema Leo February, 12,2024 wakati akifungua kikao cha maandalizi ya chanjo ya Surua kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ,ambapo amewataka Kila mmoja kwa nafasi yake kutoa elimu kwa jamii kuwalinda watoto kwakuwapa chanjo Ili kuwakinga na Surua pamoja na Rubela.
Pamoja na hayo Masindi amewataka wataalamu kutumia lugha nzuri kwa Wananchi na kuhakikisha wanakuwa waadilifu katika kazi hiyo kwani inahusu Afya, huku akiwataka kuambatana na viongozi wa Serikali za vijijini na Kata Ili kurahisisha majukumu yao .
"Nendeni mkawatumie viongozi wa vijiji ,kata na vitongoji Ili kufanikisha zoezi letu Ili tuje kujipima tumefikia malengo yetu kwa kiasi gani ‘’ Alisisitiza Das Masindi
Hyasinta Alute Muuguzi Mkuu Mkoa wa Singida, ambaye pia ni mratibu wa chanjo Mkoa aliwataka wataalamu watakaoenda kutoa chanjo kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kupata chanjo wanapatiwa ili kuwakinga na ugonjwa wa Surua ambao uliotajwa kuwepo mwaka jana katika Kata ya Mwangeza na kuwasihi kufanya kazi kwa moyo na bidii kuhakikisha wanawafikia watoto wapatao elfu 34 ndani ya Wilaya ya Mkalama.
Awali akiwasilisha taarifa , Mratibu wa chanjo Wilaya ya Mkalama Tope Webiro amesema kuwa Wilaya inakusudia kuchanja Zaidi ya Watoto elfu 34 kwenye maeneo mbalimbali ikiwepo Shule, Vituo vya kutolea huduma za Afya, Masoko , Vituo vya basi(Stendi) ambapo amesema kutakuwa na vituo 38 vya kudumu pamoja na vituo 17 vya kuhama hama hivyo kutoa wito kwa wazazi kupokea chanjo hiyo kwa mtazamo chanya ili kuwalinda watoto dhidi ya Surua na Rubela.
Chanjo hii inatarajiwa kuanza February 15-18 kwa Nchi nzima ikiwa na kauli mbiu isemayo ‘’ONYESHA UPENDO MPELEKE MTOTO AKAPATE CHANJO’’
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.