Katika kusherekea miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, timu za michezo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mkalama zimecheza michezo mbalimbali ya kirafiki dhidi ya za Halmashauri ya Igunga katika mwaliko maalumu uliondaliwa na uongozi wa michezo wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga.
Bonanza hilo lililofanyika Aprili 26,2024 lilijumlisha timu za mpira wa miguu, mpira wa nyavu pamoja na mpira wa pete.Katika mchezo wa mpira wa Pete timu Halmashauri ya Igunga iliponea chupuchupu baada ya kukubali sare goli 6-6 kutoka kwa timu ya Halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
Mchezo wa mpira wa miguu, timu hakukua na mbabe baada ya timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 huku mchezo huo ukisimama kwa dakika kadhaa kutokana na kunyesha kwa mvua. Lakini katika mchezo wa wavu, Halmashauri ya wilaya ya Mkalama ilipoteza mchezo huo kwa seti 2 dhidi ya wenyeji Halmashauri ya wilaya ya Igunga.
Tarehe 27/04/2024, Timu ya michezo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mkalama ilicheza michezo mingine dhidi ya watumishi wa Singida DC. Katika mchezo wa mpira wa miguu, Mkalama imeichapa bira huruma timu ya Singida DC goli 7-2 huku katika mchezo wa Pete ikipoteza kwa jumla ya magoli 12-6.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.