Na Rachel Joram
Baraza la madiwani wa Halmshauri ya wilaya ya Mkalama leo limepitisha mpango na bajeti ya Tsh 34,107,102,302.98 kwa mwaka fedha 2022/2023.
Bajeti hiyo imepitishwa katika baraza maalum la madiwani lilifanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
Aidha Bajeti hiyo ni kwaajili ya mishahara,matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo ambapo katika utekelezaji huo kipaumbele kikubwa ni kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Sh.1,170,000,000.00 hadi Sh.1,210,000,000.00 ambazo kati ya 40% sh.484,000,000.00 zitatumika kwa shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na 60% Sh 726,000,000.00 zitatumika katika shughuli za uendeshaji.
Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki Mhe. Isack Mtinga amesema kuwa akiwa kama mwakilishi wa Wananchi atahakikisha anaomba mafungu ya bajeti inapotokea fursa na kuaahidi kushugulikia changamoto zilizo ndani ya uwezo wake, ambapo sambamba na hayo amewataka wahemiwa madiwani kuwahamasisha wananchi katika kata zao kupanda miti kwaajili ya kutunza mazingira.
Akiahirisha kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Mhe. James Mkwega amesema kuwa Rasimu ya bajeti hii ina miongozo ya ukomo lakini bado halmashauri ina uhitataji mkubwa wa kuongezewa bajeti kutokana na halmashauri kuwa na miradi mingi ya kutekeleza kwenye sekta ya Elimu ,Afya , maji na miundombinu ya barabara.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.