Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania (TARURA) Wilaya ya Mkalama imejipanga kutumia kiasi cha fedha Tsh. 2,201,880,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za matengenezo ya Barabara kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Mkalama, Bw. Edward Masola amesema hayo Tar 27 January 2023 wakati akiwasilisha Mpango na Bajeti katika Baraza maalum la Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Aidha, Bw. Masola alisema kuwa katika fedha hizo kiasi cha Tsh. 500,000,000.00 ni kutoka Mfuko wa Jimbo, Tsh.1,000,000,000.00 ni Tozo za Mafuta , Tsh. 6,000,000,000.00 kutoka Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo
Alieleza kuwa sambamba na juhudi za Serikali kuhakikisha Barabara zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka bado kuna changamoto nyingi ikiwemo wananchi kuendelea kuswaga Ng’ombe barabarani, kuvamia hifadhi ya barabara na kufanya shughuli za kilimo na ujenzi pamoja na kuvuta majembe katikati ya barabara na kupelekea uharibifu wa barabara.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Mhe. John Mkwega aliwapongeza TARURA kwa bajeti nzuri itakayoenda kuboresha miundombinu ya Barabara ambayo itafanya Barabara kupitika kwa kipindi kirefu cha mwaka na kuwataka kuwachukulie hatua wananchi waliolima hadi kwenye hifadhi ya Barabara.
Wakala wa Barabara Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ina mtandao wa Barabara wenye urefu wa KM. 647.16, Mtandao wote huo unajumuisha aina tatu za Barabara zilizopo ndani ya Wilaya ambazo ni Barabara za Mkusanyo (Collector), Barabara za Mrisho (Feeder) Pamoja na Barabara za Jamii(Community roads).
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.