Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Mkalama limepitisha kwa kishindo bajeti pendekezwa kwa mwaka wa fedha 2024/25. Akizungumza katika baraza hilo lililofanyika Februari 13,2024 katika ukumbi wa Sheketela, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. James Mkwega ameipongeza Halmashauri samba samba na kuwataka watumishi kusimamia vizuri bajeti hiyo kama ilivyopangwa katika kuleta maendeleo kwa wananchi na wilaya kwa ujumla.
"Kwanza nawapongeza sana kwa bajeti nzuri, Nawaombeni sana, chondechonde nendeni mkasimamie bajeti vizuri. Tunaimani kubwa sana na serikali" Mhe. James Mkwega
Awali akiwasilisha mapendekezo ya hayo, Mkurugenzi Mtendaji Bi.Asia Messos amesema kwa mwaka wa fedha 2024/25, Halmashauri imepanga kukusanya na kutumia jumla ya kiasi cha shilingi 29,966,375,000.000
"Kwa mwaka wa fedha 2024/25 Halmashauri ya wilaya Mkalama imepanga kukukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni 29,966,375,000/= kwa ajili ya mishahara, matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo", Bi Asia Messos
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.