Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Mohamed Atiki amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwaletea vifaa vya kisasa vya TEHAMA vitakavyosaidia kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi wilayani Mkalama.
Kauli hiyo ameitoa Mei 23,2024 wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa vya TEHAMA kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Nduguti lililofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo halmashairi ya wilaya ya Mkalama.
“Kwanza nimshukuru Rais Dkt. Samia kwa vifaa hivi ambavyo vitatusaidia katika kujifunza masuala ya TEHAMA, vifaa hivi vitawasaidia walimu pia katika kufundisha. Nawasihi walimu na wafunzi watunze vifaa hivi ili na vizazi vijavyo viweze kunufaika na teknolojia hii” Mohamed Atiki
Kwa upande wake Afisa Elimu Takwimu Na Vifaa kwa shule za Msingi wilaya Mkalama, Mwl. Enock Lyanga amesema vifaa hivyo vitasaidia kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi wilayani Mkalama.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya Nduguti, Thuraiyaa Samihu amesema vifaa hivyo vitawasaidia kuwa wabunifu katika masomo yao,kuondoa tatizo la utoro mashuleni na kuongeza hali ya wanafunzi kujifunza zaidi.
Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na Smart TV nchi 65 pc 1, Projekta 2, Stendi ya projekta 1, Lenzi ya kamera 1, Digital Camera 1, Wireless router 1, wino, Microphone speaker 1, na mashine ya photocopy 1.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.