• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Achia shoka kamata mzinga- Nchimbi

Imewekwa kwenye: August 4th, 2017

Maadhimisho ya 21 ya Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama NANENANE yamefunguliwa rasmi jana kwa kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Singida na Dodoma.

Mgeni rasmi katika Ufunguzi huo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Daktari Rehema Nchimbi ambaye alitumia muda usipungua dakika 45 kusisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kilimo na ufugaji wenye  tija ili kuendana na falsafa ya serikali ya awamu ya Tano nayohimiza zaidi Uchumi wa Viwanda.

Mhe: Nchimbi amesema kuwa ni vizuri maadhimisho ya Mwaka huu yakaonesha mabadiliko chanya kwa washiriki waliojitokeza katika kuonesha bidhaa mbalimbali na wale waliofika kwa ajili ya kununua au kupata maelezo ya matumizi ya bidhaa hizo.

“ Nimepita kwenye banda la Jeshi la Magereza na kuona bidhaa nyingi sana zilizotengenezwa na Ngozi na wamenihakikishia kuwa kiwanda chao kina uwezo wa kununua ngozi yote inayopatikana katika Mikoa ya Singida na Dodoma hivyo ni vizuri tutumie hiyo kama fursa” Aliongeza Mhe: Nchimbi.

Mhe: Nchimbi ameliomba Jeshi la Magereza na wawekezaji wote wa ndani nan je ya Nchi wafike kuwekeza katika mikoa ya Singida na Dodoma na kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma watahakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa kila atakayekuwa tayari kuwekeza katika Mikoa hiyo.

“Kila siku huwa nasisitiza Mikoa ya Singida na Dodoma haina ukame na ndio maana hivi sasa tunataka kuanzisha mpango maalum wa kilimo cha umwagiliaji kwa sababu watafiti wameshatuhakikishia mikoa hii ina kiwango kikubwa sana cha maji ardhini tena yapo karibu sana na uso wa ardhi” Alisisitiza Mhe: Nchimbi.

Katika hatua nyingine Mhe: Nchimbi amewataka wananchi wa Mikoa ya Singida na Dodoma kuacha kabisa kukata miti kwa kisingizio cha kujikwamua kiuchumi kwa sababu kuna njia nyingi sana za kuondokana na hilo badala ya kuharibu misitu.

“Kule Singida nimeanzisha kampeni inayojulikana kama ‘ACHIA SHOKA, KAMATA MZINGA’ ambayo inampa mwananchi nafasi ya kuamua kuacha kukata mti na badala yake anafuga nyuki jambo linalomsaidia kujikwamua kiuchumi kwa muda mrefu zaidi kwa sababu unaweza kuukata mara moja tu lakini mzinga unaweza kuutundika mara nyingi kadri uwezavyo”

Mhe: Nchimbi alimalizia hotuba yake kwa kuwasisitiza maafisa kilimo kupeleka kalenda za kilimo katika ngazi zote kuanzia ngazi ya kijiji ili iwe rahisi kwa Mkulima kujua aina ya mazao anayoweza kulima kwa Mwaka husika badala ya kumsubiri Mkulima apate madhara kwanza  ndipo aje apewe elimu ya mazao aliyotakiwa kulima kwa mwaka husika.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.