Mkuu wa wilaya ya Mkalama amefanya ziara ya kikazi katika vijiji vya Mkiko na Mpambala kata ya Mpambala wilayani Mkalama kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakambili wananchi wa vijiji hivyo
Akizungumza kwa nyakati tofuati katika vijiji ya Mkiko na Mpambala, Aprili 19/2024, Mhe. DC Machali amewataka wazazi kuwapeleka watoto shule badala ya kuwaozesha na kuwapeleka kuchunga Ng'ombe
“Acheni kuozesha watoto wadogo,acheni kuwapelekea watoto kuchunga Ng'ombe, pelekeni watoto shule. Shikeni Elimu, wekeni kipaumbele katika elimu, Mimi nimefika hapa ni matunda ya elimu” Mhe. Moses Machali
“Changieni chakula watoto wapate chakula shuleni. Mtoto mwenye njaa hawezi kujifunza vizuri. Mtendaji hakikisha kila mzazi anachangia chakula” Mhe. Moses Machali
Aidha Mhe.Moses Machali amewakumbusha wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao kwani vijana wengi wamejikuta wakiangukia katika makundi hatarishi kutokana na wazazi kushindwa kufuatilia tabia zao.
Akijibu swali kuhusu ujenzi wa barabara ya Lugongo-Tatazi- Mkiko, Meneja wa TARURA wilaya ya Mkalama Mhandisi Rahabu Lukeha, amesema katika mwaka wa fedha 2024/25 serikali imeweka bajeti ya milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.