Wananchi wa Kijiji cha Ilongo , Kata ya Ibaga wametakiwa kuacha kugomea shughuli za maendeleo na kupisha taratibu za utatuzi wa migogoro yao kupatiwa suluhu na mamlaka husika.
Kauli hiyo imetolewa Januari 13,2024 na Wakili, Anton Elias kutoka Wizara ya Katiba na sheria wakati akijibu swali la wanachi hao katika kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia inayoendelea Wilayani hapa baada ya wananchi hao kumlalamikia Mayunga Ng’wigulu kuvamia eneo la malisho lililotengwa na serikali ya kijiji cha Ilongo.
“Niwaombe ndugu zangu wa Ilongo kugomea shughuli za maendeleo hakuleti suluhu ya mgogoro wenu” Alisisitiza Wakili Elias
Aidha Wakili, Elias amesema kuwa lengo la kampeni hii ni kuhakikisha wananchi wanakua na elimu ya masuala ya sheria ambapo aliwataka wananchi hao kutumia kampeni hiyo vizuri kuibua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao hivyo kufuata taratibu stahiki katika kupata haki zao.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano viongozi waliopo na kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kuendeleza maendeleo ya kijiji chao.
Baadhi ya wananchi ambao majina yao yamehifadhiwa wameiomba serikali kupitia kampeni hii ya msaada wa kisheria ya Mama Samia( Mama Samia Legal Aid Compaign) kutatua mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu ambapo wamesema takribani hekari 18 zilizovamiwa na Bw. Mayunga Ng’wigulu zinarudi mikononi mwa serikali ya kijiji kwa manufaa ya watu wa Ilongo.
Kampeni hii imeendelea leo katika Vijiji vya Mkalama, Ibaga na Ilongo katika Kata ya Ibaga
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.