Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Sophia Kizigo amesema Serikali wilayani hapa imejipanga kikamilifu kuhakikisha Wilaya inakua katika hali ya amani na utulivu na kuwaonya wote watakaojaribu kuvunja sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Ameyasema hayo Leo wakati akitoa salamu za Serikali katika kikao Cha baraza la kawaida la madiwani robo ya tatu (3).
Pamoja na salamu hizo amewataka madiwani pamoja na viongozi wa Serikali na dini kuhamasisha Wananchi juu ya ushiriki wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 Mwaka huu na kuwa zoezi hilo litasaidia Serikali kupanga bajeti kulingana na idadi sahihi ya watu pamoja na vipaumbele vilivyopo katika jamii.
Aidha Kizigo ameendelea kusisitiza kuwa Serikali itasimamia agizo lake la kupiga marufuku waganga wa tiba za asili (Lambalamba) ambao wamekuwa wakileta taharuki Kwa jamii kutokana na kupiga ramli chonganishi jambo ambalo halikubaliki.
"Tayari kuna watu waliokuwa wakijuhusisha na vitendo hivyo tumekwisha wakamata na wengine wataongezeka baada ya upelelezi kukamilika hivyo napenda kutoa onyo kwa mara nyingine kwa wale tutakao wabaini wakifanya hivyo tutaendelea kuwakamata" alisema Kizigo.
Akisisitiza umuhimu wa Sensa kitaifa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama James Mkwega alisema ni vema zoezi hilo liwafikie wananchi wa kabila la Waazabe ambao maisha yao nitofauti na watu wengine kimazingira.
Amesema kundi hilo la wananchi linapaswa kupewa elimu ya sensa ya mara Kwa mara Ili walielewe na kujitokeza Kwa wingi katika zoezi hilo ambapo Mratibu wa Sensa wilayani hapa Bw. Daniel Tesha alisema tayari mazingira mazuri yameandaliwa dhidi yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos ametaja shughuli zinazoendelea wilayani hapa kuwa ni pamoja na zoezi la Anuani za Makazi na Postikodi ambapo amewaomba madiwani kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo vizuri Ili Kila nyumba kuwa na namba.
Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki Mhe. Francis Isack Mtinga amesema kwasasa bunge la bajeti linaendelea na akiwa kana mwakilishi wa Wananchi anahakikisha wanaomba bajeti kubwa ya fedha Ili kutekeleza miradi ya maendeleo.
Aidha ameiomba Halmashauri kujenga soko la kawaida na vitunguu Ili kuinua Uchumi wa Wilaya ya Mkalama.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.