Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya Shilingi bilioni 33.955 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri aliipongeza Menejimenti kwa jitihada inazoendelea kuzifanya katika ukusanyaji wa mapato ya ndani. Aidha, aliwataka watumishi kuongeza ubunifu katika kubuni na kuimarisha vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza uwezo wa kifedha wa Halmashauri.
Akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Bajeti, Afisa Mipango, Abdallah Karoboneka, amesema baadhi ya miradi ya maendeleo itakayotekelezwa kupitia bajeti hiyo ni pamoja na ukamilishaji wa Kituo cha Afya Ilunda na uboreshaji wa stendi za Iguguno na Nduguti.

Aidha, Halmashauri inapanga kukamilisha ujenzi wa zahanati tatu katika maeneo ya Mwando, Mazangili na Isene ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mbunge wa Iramba Mashariki, Jesca Kishoa, ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mkalama kwa kazi nzuri inayofanyika katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.