Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amewataka wakazi wa Kijiji cha Mwangeza na wilayani Mkalama kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pamoja na kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Wito huo ameutoa Julai 16,2024 wakati wa ziara ya kikazi ya Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Moses Machali ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazo wakabili wananchi wa Kijiji cha Mwangeza
“Zoezi la uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura hapa kwetu litaanza Disemba 11-17,2024. tujitokeze kwa wingi hii ni haki ya msingi kwa kila mwananchi wa Mwangeza na Mkalama wa ujumla lakini pia tushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuchagua viongozi sahihi” Bi.Asia Messos
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi.Asia Messos amewakumbusha wajawazito wilayani Mkalama Kwenda kliniki mapema ili kuepuka madhara yanayoweza jitokeza wakati wa kujifungua.
“Unapofika kliniki mapema wataalamu wetu wanakuwa katika nafasi nzuri ya kufanya uchunguzi mapema na kujua hali ya mama pamoja na mtoto. Nitoe wito kina baba tuwasindikize kina mama kliniki, kifo cha mama na mtoto kinaepukika”
Vile vile Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bi. Asia Messos amewataka wazazi kuungana pamoja kukomesha tatizo la utoro kwa wanafunzi wilayani Mkalama badala yake wawapeleke watoto wao shule kwa maslahi mapana ya jamii na taifa kwa ujumla.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.