Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewataka watendaji wa Kata, watumishi wa afya pamoja na wahudumu ngazi ya jamii kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya Lishe na tamko la jiongeze tuwavushe salama pamoja bima ya afya iliyo boreshwa (iCHF) ili kuhakikisha viashiriavyote vinapata rangi ya kijani na kutoka kwenye rangi ya njano na nyekundu ili kupelekea Wilaya kuwa katika nafasi nzuri ya Lishe ndani ya Mkoa wa Singida.
Amesema hayo mapema leo February 8, 2024 kati ka kikao cha tathimini ya Lishe kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wafedha 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama.
Aidha amewataka kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake kikamilifu katika kutoa elimu ya lishe kwa jamii pamoja na kutembelea watoto chini ya miaka mitano, wamamawajawazito , elimu ya uzazi wa mpango pamoja nakuwaelimisha wazazi kuhusu kuendelea kuchangia chakula shuleni ili kutengeneza taifa la watoto wenye afya bora na wenye utimamu wa akili.
‘’Jitumeni, tusifanye kazi kwa kuvutana suala la lishe ni ajenda ya taifa hakikisheni mnaenda kutoa elimu kwa wananchi iliwaweze kufahamu suala la lishe sahihi , tamko la jiongezetuwavushe salama pamoja na bima ya afya iliyoboreshwa’’ Alisisitiza Dc Machali.
Pamoja na hayo amewaagiza kuhakikisha wanasimamia vizuri mapato ya Hospitali, Vituo vya afya na zahanati na kuwataka kujenga utamaduni wa kutembelea Hospitali kujua idadi ya wagonjwa waliopatiwa huduma katika vituo vinavyohusika ili pesa inayopatikana kutokana na matibabu hayo ziweze kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kulingana na ufinyu wa bajeti.
Awali akiwasilisha taarifa ya hali ya Lishe Wilaya ya Mkalama Afisa Lishe Wilaya ya Mkalama Zacharia Nyahende amesema kuwa kama Halmashauri imejiwekea vipaumbele kwa mwaka2023/ 2024 kuwa ni kuhakikisha kitengo cha lishe kinaendelea kuimarisha huduma za lishe hususani kwa watoto chini ya miaka mitano, vijana barehe, wanawake wenye umri wa kuzaa pamoja na wazee huku wakiendelea kupunguza tatizo la virutubisho vya vitamini na madini kwa kuhamasisha shule kutumia unga wa mahindi uliongezwa virutubisho.
Mratibu wa Afya ya uzazi na Mtoto Emmanuel Ngeleja amesema kuwa Wilaya inaendelea kuimarisha mfumo wa M-Mama katika maeneo yote ndani ya wilaya ili kumsaidia mama na mtoto na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuchukua hatua za mapema kwa mama anapojisihi uchungu hasa akiwa nyumbani, kuunda kamati zinazohusika kufuatilia wajawazito pamoja na kuendelea kuhimiza wakinamama kupata huduma ya Utrasound kwa kipindi cha ujauzito ili kubaini changamoto mapema na kuzifanyia kazi.
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.