Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amefanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kijiji cha Nkinto kilichopo kata ya Nkito wilayani Mkalama.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara, Leo Julai 29,2024 Mhe. Machali amewataka wazazi wa Kijiji cha Nkinto na wilayani Mkalama kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kupinga mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi.
“Tunawajibu mkubwa wa kumlinda mtoto wakike, wananchi wenzangu tushirikiane pamoja kupambana dhidi ya tatizo la mimba mashuleni. Nawaomba sana mtoe ushirikiano pindi kesi za mimba zinapofika Mahakamani, wanaume achaneni na wanafunzi” Mhe. Machali
Mhe. Machali amesisitiza kuwa mzazi yeyote atayebainika kuwa chanzo cha kukwamisha Ushahidi mahakamani atachukuliwa hatua za kisheria “Mtendaji kuanzia leo ikiwa kuna mzazi anahusika nayeye achukulie hatua za kisheria” Mhe. Machali
Akijibu swali kuhusu changamoto ya maji iliyoibuka wakati wa mkutano huo wa hadhara, Mhe. Machali amesema tayari serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kuleta maji safi na hata wataalamu kutoka Mamlaka ya Bonde la Maji mkoa wa Singida wapo Kijiji Nkinto kufuatilia vyanzo vya maji.
“Niwahikishishie wananchi wa Kijiji cha Nkinto na vijiji vya Jirani kuwa tayari watalaamu wetu wako kazini nimekujanao hapa, mwaka huu hautaisha mtakuwa mmepata Maji” Mhe. Moses Mahali
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.