WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Wananchi wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida kuzitunza barabara zilizojengwa na Serikali kwa gharama kubwa.
Mhe. Ummy ametoa ombi hilo wakati akizungumza na wananchi hao wakati akikagua barabara ya Singa- Kinampundu-Ilunda iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe katika ziara ya kikazi ya siku moja aliyoifanya wilayani hapa ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Elimu, Afya na Miundo mbinu ya Barabara.
"Jambo lililokubwa nawaomba wananchi mzitunze hizi barabara kwa sababu Serikali inazichonga lakini kunawananchi wanapitisha majembe ya kukokotwa na ng'ombe kwa hiyo niombe ulinzi wa barabara uwe ni jukumu letu sote kwa sababu fedha zilizotumika kuzitengeneza ni nyingi hivyo tunatamani ziendelee kuwa na ubora na zisaidie kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi" alisema Waziri Ummy.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijiji wa Wilaya ya Mkalama, Edward Masola amesema matengenezo ya barabara hiyo yatagharimu kiasi cha Sh.milioni 91,201,000.
Aidha ameendelea kuwa barabara hiyo ambayo inaunganisha Kata za Ilunda na Kinampundu itakapokamilika itarahisisha usafiri kwa wananchi kufikia huduma za elimu, afya na masoko.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy ametembelea Ujenzi wa kituo cha Afya cha Ilunda kilichopo Kata ya Ilunda ambapo amefurahishwa na Kasi ya Ujenzi huo na kushiriki shughuli za ujenzi katika kituo hicho.
Awali akitoa taarifa ya kituo hicho cha afya, Mganga Mkuu wa wilaya Dr.Ibrahim Pazia amesema fedha za ujenzi wa kituo hicho ni Sh.mill 250,000,000 zilizotokana na tozo na kuwa kitakuwa na majengo matatu jengo la wagonjwa wa nje (OPD) jengo la maabara na kiteketeza taka.
Amesema mradi huo utakapo kamilika utahudumia wananchi 12,000 wa vijiji vya Asanja, Nkungi, Ilunda na Iambi, Kinandili , Nduguti na vijiji jirani vya Mkunguru, Kidigida na Kata ya Kinampundu.
Sanjari na hayo Mhe.Ummy Mwalimu ametembelea kikundi cha Vijana Iguguno kijulikanacho kama (Youth Group) kinachojishughulisha na ufyatuaji wa tofali pamoja na ufugaji wa Kuku wa kienyeji ambapo aliwachangia kiasi cha sh.Mill.2 huku Mkuu wa Mkoa Dkt.Binirith Mahenge naye akichangia kiasi hicho cha fedha ili kuwauunga mkono katika ufugaji wa Kuku.
Pia Waziri Ummy ametembelea Ujenzi wa zahanati ya Kisuluiga iliyopo Kata ya Gumanga ambapo ameiomba Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kutoa kiasi cha sh.Mill 60 ili kukamilisha Ujenzi huo ambapo ikikamilika itahudumia zaidi ya watu 3000 pamoja na hayo ametembelea Ujenzi wa madarasa 7 katika Shule ya Sekondari Gumanga uliogharimu kiasi cha sh. mill.140,000,000.
Naye Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki Mhe.Fransis Isack Mtinga ameishukuru serikali ya awamu ya sita kutoa fedha kwaajili ya miradi ya Maendeleo ambapo amemuahidi Mhe . Waziri kuwa watasimamia vizuri fedha hizo ili kuhakikisha inakamilisha miradi iliyokusudiwa ndani ya Wilaya ya Mkalama .
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.