• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WA MIGANGA NA NKALAKALA WAHIMIZWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Imewekwa kwenye: September 5th, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama amewataka wakazi wa kata za Nkalakala na Miganga wilayani Mkalama kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali Za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024

Wito huo ameutoa Septemba 4,2024 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata hizo wilayani hapa.

“Mwaka huu tutakuwa na zoezi kubwa la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024, tujitokeze kwa wingi wetu tushiriki uchaguzi huu kwa maendeleo ya kata zetu. Usikubali mtu mwingine akuchagulie kiongozi wakati unauwezo wa kupiga kura” DED Asia Messos

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi.Asia Messos amesema kuwa ili mwananchi aweze kupiga kura siku ya Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, anapaswa kujiandikisja katika daftari la Orodha ya Wapiga Kura ambapo zoezi la uandikishaji litafanyika kuanzia Octoba 11-20,2024

Aidha Bi. Asia Messos amewataka wanawake wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi huo kwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili waweze kushiriki katika maamuzi yatayoleta maendeleo ndani ya kata zao “Kina mama tujitokeze kwa wingi kuchukua fomu tuwe na viongozi wanawake kwenye nafasi za maamuzi” Bi. Asia Messos

Akizungumzia kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Bi. Asia Messos amesema zoezi hilo kwa mkoa wa Singida linatarajia kufanyika Septemba 25,2024 na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhuisha taarifa zao na ambao hawana kadi wajitokeze kwa wingi kujisajiri ili wapate kadi ya mpiga kura

Awali akieleza mambo makubwa yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita katika miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bi. Asia Messos amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imepokea zaidi ya Bilioni 60 kwa ajili ya miradi mbalimbali kama vile elimu, afya, michezo, kilimo.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.