• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Tanzania kuongoza Afrika katika usambazaji wa umeme

Imewekwa kwenye: April 14th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt .Binilith Mahenge amesema Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Barani Afrika  kwa kusambaza umeme katika vijiji vyote.


Dk. Mahenge ameyasema hayo  wakati akizungumza na wananchi wa Kata za Gumanga,  Iguguno na , Tumuli Wilaya ya Mkalama katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa  katika Sekta ya Afya, Maji na Elimu.


Miradi aliyoitembelea na kuikagua ni ujenzi wa shule mpya ya Sekondari inayojengwa Kitongoji cha Kisubio katika Kata ya Iguguno ambapo ujenzi wake utagharimu Sh.600 Milioni, ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Gumanga Sh.500 Milioni ambapo wamepokea nusu yake Sh.250 Milioni na mradi wa maji uliopo katika Kijiji cha Milade ambao utagharimu Sh. 502 Milioni.


"Tumshukuru sana Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan huyu  mama ni wa mfano kwani ametoa fedha zaidi ya Sh. 60 Bilioni kwenye eneo la umeme amini usiamini Tanzania tutakuwa wa kwanza kwa kusambaza umeme vijiji vyote Barani Afrika ifikapo 2025" alisema Mahenge huku akishangiliwa.


Alisema katika wilaya  vijiji vyote ambavyo havina umeme kuna mkandarasi yupo kazini akiweka miundombinu ya umeme ambao ukikamilika utatoa fursa kwa wananchi kuweka mashine za kusaga, saluni za kike na kiume na biashara zingine mbalimbali zinazotegemea umeme.


Alisema Mkoa wa Singida una vijiji 441 na kati ya hivyo 176 vilikuwa havina umeme lakini sasa vijiji vyote hivyo Rais Samia Suluhu Hassan anaweka umeme ambapo alisema ni  jambo kubwa la kujivunia ambalo halijawahi kutokea hapa nchini na kuwa tayari kuna wakandarasi wawili wanafanya kazi mmoja anahudumia  Wilaya ya Iramba na Mkalama na mwingine anahudumia Wilaya ya Ikungi, Manyoni na Singida Vijijini.


Alisema katika Mkoa wa Singida Rais Samia ametoa zaidi ya Sh.232 Bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kati ya fedha hizo Sh. 30 Bilioni zimeelekezwa kwenye eneo la elimu ambapo shule mpya 9 zinajengwa kwa wakati mmoja.


"Mbali ya ujenzi wa shule hizo kuna zahanati zinajengwa, vituo vya afya, barabara na kwa Wilaya ya  Mkalama tayari daraja kubwa la Msingi ambalo limegharimu Sh.10 Bilioni limejengwa ambalo litawaunganisha na Mkoa wa Simiyu na Meatu hivyo kutimiza hoja ya kuwaletea wananchi wa Mkoa wa Singida na Wilaya ya Mkalama maendeleo" alisema Dk. Mahenge.  


Diwani wa Kata ya Gumanga  na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama  Mhe. James Mkwega  ameshukuru kwa upatikanaji  wa kituo hicho cha Afya  ambapo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Sh.500 Milioni kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Gumanga  ambapo alimuomba mkuu wa mkoa kumpelekea shukurani hizo.


"Sisi Wana Gumanga hatuna cha kusema shida yetu kubwa ilikuwa ni kupata kituo cha Afya ambacho kitawapunguzia adha wanananchi hasa wakina mama ambayo walikuwa wakiipata kwa kutembea umbali mrefu wa kilometa 33 kufuata huduma hiyo Kituo cha  Afya cha Kinyambuli " alisema Mkwega.


Alisema walikuwa na uhitaji mkubwa sana wa kituo hicho kwani kuna wananchi wa Kitongoji  cha Kitulamando wapo umbali wa kilometa 25  Kijiji cha Mgimba  na  Kinankamba ambao wapo kilometa 30 waliokuwa wakitembea umbali huo kufuata huduma ya afya katika Zahanati ya Gumanga.


Mkwega alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutasaidia wananchi zaidi ya 18,000 kutoka katika maeneo hayo kupata huduma kwenye kituo hicho cha Afya cha Gumanga ambacho kitakuwa kikitoa huduma ya Uzazi,  Upasuaji na jengo la kufulia.


 Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo alisema wilaya itakua  na vituo vya afya vitatu ambavyo amevitaja kuwa ni cha Mkalama, Ilunda na cha Gumanga ambacho fedha zake tayari zimepokelewa.


"Hili ni jambo kubwa alilolifanya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwani katika kipindi chake cha uongozi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja katika wilaya yetu ya Mkalama anatujengea vituo viwili vya afya vitakavyokuwa na sifa ya upasuaji hakikika ni kazi kubwa aliyotufanyia tunakila sababu ya kumshukuru na kumpongeza" alisema Kizigo .


Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Uchimbaji wa Msingi wa ujenzi wa kituo Cha afya Gumanga kata ya Gumanga, ujezi wa shule ya Sekondari mpya kitongoji Cha  Kisubiu kata ya Iguguno pamoja na Mradi wa Maji kijiji cha Milade kata ya Tumuli.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.