Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Mkalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Moses Machali, leo January 31, 2024 imetembelea mgodi wa madini wa Pubo uliopo kata ya Tumuli wilayani Mkalama kwa ajili ya kukagua shughuli za uchimbaji zinazofanywa katika mgodi huo.
Mara baada ya kumaliza ukaguzi na kujionea shughuli za uchimbaji, Mhe. Machali ameutaka uongozi kufuata taratibu na sheria zilizoweka na serikali za uchimbaji madini ikiwemo kulipa mapato ya Halmashauri
"Kwanza naowamba muilipe Halmashauri fedha za mawe tani 1500 mlizopeleka Iramba kwa ajili ya kuchakatwa, pia nawaomba kwasasa msitishe zoezi la uchimbaji shimo la taka sumu kwa muda ili mfuate taratibu zilizowekwa ili kupusha hasara inayoweza kujitokeza kutokana na kukiuka tararibu. Tunataka mgodi ukuwe, ajira ziongozeke na mapato yaongezeke pia" Mhe. Moses Machali
Aidha Mhe. Moses Machali ameuagiza uongozi wa mgodi kudumisha uhusiano na jamii zinazoishi karibu na mgodi huo
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.