Mkuu Wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo amewataka wananchi wilayani hapa kuendelea kutoa taarifa zote sahihi zikiwemo za watu wenye makundi maalum ili kufanikisha zoezi la sensa linaloendelea nchini.
DC Kizigo amesema hayo Leo agosti 23 baada ya kuhesabiwa akiwa nyumbani kwake ambapo amesema zoezi la sensa katika Wilaya limeenda vizuri.
"Zoezi la sensa katika Wilaya yetu limeenda vizuri sana, tumeanza saa 6 usiku Wa kumkia Leo tarehe 23 tumehesabu watu Wa makundi maalum wakiwemo Mahabusu,watoto Wa mtaani, wagonjwa hospitalini na familia mbalimbali tunawashukuru makarani wetu kwa kufanya kazi nzuri na tunawaomba waendelee mpaka zoezi Litakapokamilika" Alisema Dc Kizigo.
DC Kizigo amesisitiza kwa kuzitaka familia ambazo hazijafikiwa na makarani siku ya Leo kutunza taarifa zao sahihi ili makarani watakapo wafikia waweze kufanikisha zoezi hilo Kwa urahisi .
"Nitoe wito kwa wananchi wote ambao hawatafikiwa na makarani Leo basi watunze taarifa zao ili kukamilisha zoezi hili muhimu kwa ustawi wa taifa letu". Alisema DC Kizigo.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Mesoss amesema zoezi la kuhesabu familia ya jamii ya Wahadzabe limefanikiwa kwa asilimia mia moja Mara baada ya kutenga bajeti ya kuwatafutia nyama jamii hio inayoishi kwa kwakutegemea shughuli za uwindaji , kula asali ,matunda pori pamoja na mizizi .
" Tunashukuru tumefika katika kitongoji hiki cha Kipamba hapa Mkalama, kuangalia zoezi hili la sensa linavyoenda tuliona kuwa jamii hiii inategemea sana nyama na asali tukaona tutenge bajeti ambapo tumewapatia ng'ombe na wamehesabiwa kisha wakala nyama zoezi limefanikiwa kwa aslimia 100%." Alisema Mkurugenzi Asia Messos .
Alisema jamii hiyo ya Wahadzabe inaishi kwa kutegemea uwindaji na asali mizizi na matunda pori hivyo waliamua kuwapatia nyama ili wabaki kuhesabiwa majumbani mwao.
"Jamii hii inajihusisha na uwindaji ni watu ambao hawatunzi chakula wala hawalimi kwahiyo tumeona tulete nyama ambayo ndio chakula chao ili kufanikisha zoezi hili muhimu kwa ustawi Wa serikali yetu". Aliongeza Bi Messos .
Baadhi ya wananchi ambao ni jamii ya Wadzabe wameshukuru serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya mkalama kwa kuwafanyia zoezi la sensa pamoja na kuwapatia nyama na kuiomba serikali kuwasaidia kulinda utamaduni wao pamoja na kuwapatia huduma za kijamii .
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.