Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amewapongeza Wauguzi wa Afya Wilayani Mkalama kwa kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya sekta ya Afya wilayani Mkalama na kwa taifa kwa ujumla
Pongezi hizo amezitoa Mei 29,2024 wakati wa sherehe ya maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani kiwilaya iliyofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
“Sijawahi kusikia hata siku moja kituo cha Afya kimefungwa kwa kukosa Wauguzi,hii ni kwasababu kazi kubwa inafanyika huko chini. Hatujawahi kukosa huduma Afya Mkalama, nawapongeza sana kwa hili” DED Asia Messos
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Bi.Asia Messos amewataka Wauguzi hao kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kama kiapo cha kazi kinavyosema
“Muendelee kufanya kazi kwa uamifu kama kiapo chenu kinavyosema, Tuchape kazi, hakuna aliyefanikiwa kwa kuwa chawa, kila aliyefanikiwa amefanya kazi, Nchi yetu haiwezi kujengwa na mtu yeyote isipokuwa sisi” Bi. Asia Messos
Kwa upande wake Mganga Mkuu wilaya ya Mkalama, Dkt. Solomon Michael amewapongeza kwa kuadhimisha siku hii muhimu kwao huku akiwataka kuendelea kuishi katika kiapo cha kazi kwa kufanya kazi kwa bidi na kwa uaminifu.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.