Wilaya ya Mkalama imeungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Watanzania wote kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kufanya shughuli mbalimbali za Maendeleo Wilayani hapa kwa kupambana miti takribani 700 katika kituo cha Polisi Cha Wilaya pamoja na Hospital ya Wilaya ya Mkalama.
DC Moses Machali
Akizungumza mara baada ya kuhitimisha zoezi la upandaji miti katika kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru ambayo huadhimishwa kila Disemba 9 ya kila mwaka, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewataka wananchi pamoja na watumishi kuwa wazalendo kwa Nchi kwa kujituma na kuwajibika kwa taifa lao kwakufanya kazi kwa bidii kwaajili ya masilahi mapana ya Nchi yao.
DAS Peter Masindi
“Hatuwezi kupata maendeleo kama hatufanyi kazi, juzi mkuu wa mkoa ametuelekeza njia pekee ya kuhakikisha tunapata maendeleo ni kwa kufanya kazi, Kila kaya inakuwa na angalau hekari mbili, katika msingi huo tunaweza kuleta mabadiliko ambayo tunahitaji”, Mhe. Machali
“Mtumishi wa serikali, mtumishi katika 'private sector' unapokuwa unafanya kazi je, masaa yote ambayo umepangiwa kufanya kazi unayatumia vizuri kuweza kuzalisha kwa ajili ya taifa lako? Watu tumepata Uhuru lakini tunauchezea, watu wanafanya uhuni mahali pakazi.Tubadili tabia zetu, tuwajibike ili tuweze kusukuma maendeleo ya taifa letu”. Alisisitiza Machali
Naye katibu tawala wa Wilaya ya Mkalama, Peter Masindi amewataka wakazi wa watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo Nchini sambamba na kuendelea kuienzi siku hii muhimu ya Uhuru kwa watanzania kuwakumbuka wazee, viongozi waliojitolea kwa ajili ya Uhuru wa taifa la Tananyika
"Tumefanya hili tukio kwa ajili ya kukumbushana kwamba tuliumia, waliumia na sisi tuumie kwa ajili ya wengine,tusiache hii tarehe ikapita kama ilivyokuja, tarehe itabadilika, lakini maendeleo na amani ya nchi yetu tuendelee kudumisha” DAS Peter Masindi.
Maadhimisho haya yanaambatana na uzinduzi wa dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025-2050 ,Kauli mbiu ya uhuru Mwaka 2023 ni "Miaka 62 ya Uhuru umoja na mshikamano ni chachu ya Maendeleo ya Taifa letu
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.