• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

DCC ya kwanza yafanyika Mkalama

Imewekwa kwenye: June 5th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka leo ameongoza kikao cha kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC)  ambapo katika hotuba yake ametoa maelekezo mbalimbali kwa wadau na idara mbalimbali zilizopo Wilayani Mkalama.

Kikao hicho mbali na kuhusisha baraza lote la Madiwani, pia kilihusisha taasisi mbalimbali zinazoendesha shughuli zake Wilayni Mkalama, Watendaji wote wa kata, wawakilishi wa taasisi za dini na wawakilishi wa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali.

Mhe. Masaka aliwataka wananchi na viongozi kutambua umuhimu wa wingi wa fedha zinazotolewa na serikali katika kuhudumia Eimu nchini kwa kuhimiza watoto kwenda shule, walimu kufanya kazi pindi wawapo shuleni na wazazi kuonesha mwamko wakati wa kuchangia huduma mbalimbali za uboreshaji wa Elimu za watoto wao.

“Jambo la pili nitumie fursa hii kuhimiza wakulima wote walime mazao ya mkakati ambapo kwa Wilaya yetu mazao hayo ni pamba, korosho, alizeti na Vitunguu” Aliongeza Mhe. Masaka.

Mhe. Masaka alisisitiza kuwa ili kilimo cha Mkakati kiweze kuwa na tija ni lazima wakulima watumie mbegu bora, wapande mazao yao kwa vipimo sahihi na watumie vipimo stahili katika uwekaji wa dawa za kuua wadudu wanaoathiri mazao hayo.

“Mawakala wa huduma za Misitu nchini (TFS) na idara ya Maliasili ni lazima waonekane wapo badala ya kuziachia serikali za vijiji  kesi za uvamizi wa maeneo ya misitu ingawa pia vijiji vyote vinapaswa kulinda maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya misitu” Aliongeza Mhe. Masaka.

Mhe. Masaka alitumia fursa hiyo kusisitiza wananchi wajenge viwanda vidogo kama  viwanda vya kukamua mafuta ya Alizeti na kuagiza kila mtu awaunge mkono wenye viwanda hivyo ili wafanikiwe na hatimaye waweze kufungua viwanda vikubwa.

“Sio Afisa afya anaenda kukagua kiwanda na kukuta mazingira yasiyoridhisha lakini badala ya kushauri namna ya kuboresha mazingira hayo anaamua kuchukua uamuzi wa kukifunga kiwanda hicho” Alisisitiza Mhe. Masaka.

Katika  hotuba yake Mhe. Masaka pia  alizitaka taasisi zote zinazofanya shughuli zake Wilayani Mkalama kuwa na mipango yenye mwelekeo mmoja ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za msingi kwa wakati badala ya huduma moja kusubiri uwepo wa huduma nyingine.

“Sio Tarura wanajenga barabara Kinyambuli, Halmashauri inaenda kujenga kituo cha Afya Gumanga, Tanesco wanapeleka umeme Kinyangiri na Idara ya Maji wanapeleka maji Ibaga, hapo mtakuwa hamjamsaidia mwananchi kwa sababu hata mkimpelekea kituo cha Afya kizuri, kama hakuna barabara nzuri kufika kwenye kituo hicho au umeme wa kutumia kituoni hapo itakuwa ni kazi bure” Alisema Mhe. Masaka.

Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Masaka aliwaomba wananchi na taasisi za dini zilizopo wilayani Mkalama kuisaidia serikali kwa kutoa maeneo ambayo hawayatumii ili yatumike katika shughuli za Maendeleo.

“Msiishie tu kumiliki maeneo hayo bila kuyaendeleza kwa kufanya shughuli za Maendeleo hivyo kama ni kilimo limeni, kama ni viwanda wekeni viwanda na kama mlipanga kuweka taasisi za Elimu wekeni taasisi hizo” Alimalizia Mhe. Masaka.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.