Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Moses Machali amewataka wazazi wilayani Mkalama kuhakikisha wanapeleka watoto wao katika vituo vya afya kupatiwa chanjo ya Surua na Rubella ili kuepuka madhara yanayowezajitokeza ikiwa mtoto hatopata huduma hiyo mapema.
Agizo hilo amelitoa Februari 15,2024 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo iliyofanyika katika hospitali ya wilaya ya Mkalama na kushuhudiwa na wakuu mbalimbali wa Idara, watumishi wa Afya pamoja na wananchi walioleta watoto wao kwa ajili ya huduma ya chanjo.
“Chanjo hizi ni safi na salama,kuwa mjanja peleka mwanao akachanjwe, itakuwa jambo la ajabu kutompeleka mtoto wako kupatiwa chanjo. Viongozi wa serikali wa vijiji hakikisheni mnahamasisha wananchi ili tuweze kufikia lengo lililowekwa na serikali” Mhe. Moses Machali
Awali akizungumza kuhusu kampeni hiyo ya chanjo, Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Solomon Michael amesema kampeni hiyo ya chanjo inatarajia kufikia watoto takribani elfu 34818 huku akiwataka kila mzazi anamleta mtoto kituo cha afya kupatiwa huduma hiyo.
“Zoezi hili litachukua siku 4 kuanzia Februari 15-18,2024 na tunatarajia kufikia watoto elfu 34818, ugonjwa wa Surua ni hatari sana. Wazazi tujitahidi kuwaleta watoto wetu katika vituo vya afya waweze kupata chanjo ya Surua ambayo ni salama kabsa”, Dkt. Solomon Michael
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.