• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

DC MACHALI AAMURU KUWEKWA NDANI MTENDAJI NA MKUSANYA MAPATO KIJIJI CHA IGUGUNO

Imewekwa kwenye: August 18th, 2023

DC MACHALI AAMURU KUWEKWA NDANI MTENDAJI NA MKUSANYA MAPATO WA KIJIJI CHA IGUGUNO


Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe Moses Machali Leo Agosti 18 ameamuru kuwekwa ndani Mtendaji wa kijiji Cha Iguguno Kiraka Monge, Kata ya Iguguno  pamoja na Mkusanya mapato wa kijiji  hicho Manase  Kizula   kwakosa la kukusanya ushuru kwa Wananchi bila kuwapa risti.

Mhe. Machali ametoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo  Agosti 18, 2023 kwenye Kata ya Iguguno ambapo alitumia fursa hiyo  kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa kata hiyo.  


"Mhe. Mkuu wa Wilaya  sisi wajasiriamali wadogo wadogo tunaojulikana kama wachuja nafaka tumekuwa tukilipa ushuru wa bidhaa zetu tangu Mwaka 2019  lakini hatujawahi kupewa  Stakabadhi ya Malipo ( Risti)" Alisema mmoja wa wafanyabiashara hao


Kutokana na Sakata hilo Mkuu wa Wilaya alimuagiza Afisa Utumishi Wilaya ya Mkalama kushughulikia watendaji wote wanaokiuka maadili ya Utumishi wa umma ambapo amesisitiza atahakikisha anapambana na wabadhilifu wote ili kila mtumishi aweze kutenda haki kwa Wananchi.


Pamoja na hayo Mhe. Machali  alimtaka Kaimu Mtendaji wa Kata ya Iguguno Paul Grindai  kuhakikisha anaanzisha mchakato wa kupata baraza la ardhi la kata baada ya lile lililokuwepo awali kuvunjwa kutokana na  kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.


" Toa tangazo kwenye mbao za Matangazo Ili Wananchi wenye sifa za kuwa wajumbe wa Baraza la Ardhi la Kata  kugombea nafasi hizo Ili kuhakikisha migogoro ya Ardhi inaanza kutatuliwa ngazi ya Kata kabla ya kwenda ngazi ya Wilaya" Alihitimisha Mhe. Machali.


Ziara ya Mhe. Machali kwenye Kata ya Iguguno  ni mwendelezo wa ziara zake za kusikiliza na kutatua kero za wananchi Wilayani Mkalama.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.