Namna ya kujiunga na CHF
Unaweza kujiunga kama kaya,mtu binafsi au vikundi na kupatiwa kadi ya uanachama. Kila kaya(familia) itachangia kiasi kitakachokubaliwa kwa mwaka, mfano(5,000 au 10,000 au 15,000)
Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi, je ninaweza kujiandikisha na familia yangu katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ?
Ndiyo, kama una wategemezi wa ziada ambao hawajasajiliwa katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Je wanafunzi wanaweza kujiunga?
Ndiyo, unaweza kuhudumia watoto katika familia,hii ikiwa ni watoto walioko katika kaya iliyojiandikisha ambao umri wao ni chini ya miaka 18.
Je naweza kujiunga kupitia kikundi cha uzalishaji au ushirika?
Ndiyo, unaweza ili mradi mkubaliane katika kikundi na uongozi wenu uwasiliane na Mganga Mkuu wa Wilaya au Mganga Mfawidhi wa kituo cha matibabu kinachohudumia wanachama wa CHF kilicho karibu.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.