ZOEZI LA KITAIFA LA UTAMBUZI USAJILI NA UFUATILIAJI WA MIFUGO
Tumepokea maelekezo toka Ofisi ya Makamu wa Rais kuwa Ng'ombe wote nchini wanatakiwa kuwekwa chapa na kusajiliwa ili kutekeleza matakwa ya Kisheria (sheria na 12 ya mwaka 2010 ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji mifugo). Katika zoezi hili Halmashauri ya Wilaya inawajibika kugharamia zoezi hili ili liweze kuleta Tija.
Katika zoezi hili mfugaji atatakiwa kulipia kila Ng'ombe Tshs 500/= ili fedha hizo zisaidie katika gharama za utekelezaji wa zoezi hili. Ng'ombe watakaohusika ni kuanzia ndama wa miezi sita na kuendelea.
Usajili huu utafanyika kwa kutumia code ambazo zimetolewa na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi ambazo ni T MKL na code za Kijiji zitatolewa na Wilaya ambapo Vijiji vitapangwa kwa kufuata Alphabeti kuanzia Kijiji namba 1 hadi 70 na chapa hiyo itawekwa mguu wa nyuma wa kulia.
Kabla ya zoezi hili inatakiwa wafugaji wote wasajiliwe na mifugo waliyonayo ndipo zoezi lianze.
UMUHIMU WA ZOEZI HILI
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi: +255 758 954 045
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.