• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkalama ni nkulu kuliko Iramba-RC

Imewekwa kwenye: June 3rd, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Daktari Rehema Nchimbi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa kupata hati safi kufuatia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mhe Nchimbi ametoa pongezi hizo muda mfupi uliopita alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano wa baraza la madiwani utakaojikita katika kujadili na kuzipatia ufumbuzi hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mhe. Nchimbi amebainisha kuwa hati hiyo haitokani na viongozi wa Mkoa au Wilaya pekee bali ni matokeo ya ushirikiano baina ya viongozi, watendaji na wananchi wa Wilaya ya Mkalama kwa ujumla.

“Wilaya ya Mkalama ni kama timu ya mpira wa miguu ambapo ili ishinde ni lazima kila mchezaji kwenye nafasi yake atimize wajibu wake na katika hili wananchi pia ni sehemu kubwa sana ya timu hiyo kwa sababu wao si tu wachezaji bali huwa ni washangiliaji pale wanapoona mambo ni mazuri lakini pia huwa ni waamuzi pale wanapoona mambo hayapo sawa ” Alisisitiza Mhe. Nchimbi.

Mhe. Nchimbi amewataka viongozi na watendaji  mbalimbali wa Wilaya ya Mkalama kuitumia ripoti hiyo ya CAG kama kioo cha kuondoa madoa mbalimbali yaliyobainishwa ndani yake ili kwa mwaka ujao wa fedha Halmashauri hiyo iweze kupata hati safi isiyo na madoa.

“Lakini pia nitumie fursa hii kuwapongeza kwa kuwa na ukumbi mzuri na wa kisasa wa mikutano na kwa hili ninaungana nanyi kuwa “Mkalama Nkulu kuliko Iramba” (Mkalama ni kubwa kuliko Iramba). Alimalizia Mhe. Nchimbi.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2020 January 16, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA NNE 2020 January 16, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2020 January 16, 2021
  • KWA WAFUGAJI WA NG'OMBE WILAYANI MKALAMA April 03, 2017
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mkalama ni nkulu kuliko Iramba-RC

    June 03, 2019
  • Mkalama yazindua bima ya afya iliyoboreshwa

    May 07, 2019
  • Wiki ya maji yafikia tamati leo Mkalama

    March 21, 2019
  • Mwakyembe afika bomani

    March 12, 2019
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Maeleo ya fomu ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mwongozo wa jinsi ya kujaza fomu za Opras
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
  • MATOKEO YA MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA NNE
  • MATOKEO YA MTIHANI WA UPIMAJI KIDATO CHA PILI

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    MKALAMA DISTRICT COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964000

    Simu ya Mkononi: +255 714 772 300

    Barua pepe: ded.mkalamadc@singida.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.